Friday, June 15, 2012

HIFADHI YA SERENGETI YAWAVUTIA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO WA SERIKALI!

Baadhi ya maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili kwenye lango la kuingia hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Maafisa habari wakipata kifungua kinywa katika eneo la Lamadi lililopo mkoa mpya wa Simiyu wakiwa njiani kuelekea katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mfanyabiashara wa supu katika eneo la Lamadi mkoani Simiyu Bw. Sobia Majuto akiwahudumia baadhi ya wateja wake ambao ni maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali walipokua njiani kuelekea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Wanyama aina ya Twiga ambao ni moja ya vivutio vikuu katika hifadhi ya taifa ya Serengeti wakitembea kwa mstari ndani ya hifadhi hiyo.
Kundi kubwa la Nyumbu wakiwa katikati ya Barabara ndani ya hifadhi hiyo na kuufanya msafara wa magari yaliyowabeba maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kwenda kwa mwendo wa polepole. Kwa mujibu wa taratibu za hifadhi ni kosa kwa dereva kupiga honi, kuendesha gari kwa mwendo kasi au kupiga honi ndani ya eneo la hifadhi.
Mnyama aina ya Simba maarufu kwa jina la mfalme wa mwitu akipanda mti ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwafanya maafisa Habari na Mawasiliano wa serikali kushangaa uwezo wa Simba huyo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment