Monday, April 30, 2012

WAZIRI GHASIA AZITAKA ASASI ZA KIIMANI KUHUBIRI AMANI, UPENDO, MAELEWANO NA MSHIKAMANO!


Tanzania imeendelea kusisitiza mashirika ya kiimani, kuhubiri amani, upendo maelewano na mshikamano baina ya waumini wake na waumini wa imani nyingine zate ili kujenga jamii inayoenzi amani, upendo, ushirikiano na mshikamano kama msingi mkuu wa maendeleo na ustawi wa jamii yetu.

Rai hiyo, imetolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hawa Ghasia, wakati wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 75, kwa Jumuiya ya Brahma Kumaris ya Upanga jijini Dar es Salaam, yaliyofanyikia ukumbu wa Utamaduni wa Urusi hapa jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ghasia, ameipongeza jumuiya hiyo kutimiza miaka 75 na pongezi zaidi ni kwa jumuiya hiyo kuhubiri amani, upendo na maelewano baina ya dini mbalimbali kwa kutumia msingi mkuu wa jumuiya hiyo kuwa Mungu ni mmoja na ni Yule Yule kwa dini zote japo anaitwa kwa majina tofauti tofauti.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Brahma Kumaris hapa nchini, Sister Lalika Patel, amesisitiza Brahma Kumaris ambayo imekuwepo nchini kwa kipindi cha miaka 26, sio dini, bali ni jumuiya ya kimaani inatoa mafundisho ya kutafakari kwa makini (meditation) hivyo kuimarisha zaidi imani za watu wa dini mbalimbali kwa kuhubiri Mungu ni mmoja.

Katika maadhimisho hayo, mtaalamu bingwa wa mambo ya meditation kutoka nchini Urusi, Sista BK Chakradali aliendesha mhadhara wa somo la kujitambua kwa kuwasisitiza waumini wa dini mbalimbali kwanza wanapaswa kujitambua wao ni nani wametoka wapi na wameumbwa kwa madhumini gani ndipo watakapo weza kumtambua mungu wa kweli.

Sister Chakradali akasisitiza watu wengi wanakiogopa kifo kwa kukosa ufahamu kuhusu mwili wa binadamu ya kuwa una semu mbili ya mwili na roho, kinachokufa ni mwili tuu, hivyo binadamu wakielimika, hawatakuwa na sababu ya kukiogopa kifo bali watajiandaa vyema kupokea kifo kwa sababu watakuwa wamepata ufahamu ni nini kinaendelea baada ya kifo cha mwili.

Watanzania mbali mbali wa dini tofauti, walitoa ushuhuda jinsi mafunzo hayo ya meditation yanayotolewa na watu wa jumuiya hiyo yalivyowasaidia kubadili maisha yao.










No comments:

Post a Comment