Thursday, January 26, 2012

VILLA SQUAD KULIPA KISASI I KWA TOTO?.

Na: ENDREW CHALE.




 Afisa Habari wa Villa Squad-ANDREW CHALLE.


TIMU ya soka ya Villa Squad Fc ‘Kambimoto’ ya Magomeni Kinondoni, Jaijini Dar es Salaam, imeingia mawindoni kwa mazoezi makali kwa ajili ya kuikabiri Toto Africa ya Mwanza, katika mchezo utakaochezwa Januari 28, uwanja wa Chamazi.

Akizungumza mapema leo, Ofisa habari wa Villa, Andrew Chale alisema timu yao licha ya kupoteza mchezo huo wa kwanza wa raundi ya lala salama, kwa kufungwa goli 4-2 dhidi ya Kagera Sugar, watahaakikisha wanapigana kiume ilikufuta uteja kwa Toto ambao mzunguko wa kwanza waliifunga Villa goli 3-1.

“Kwa kuwaambika tu mashabiki na wadau wa Villa, tusikate tama na zaidi ni kuongeza ushirikiano ilikuongeza morali kwa wachezaji na kocha kwani timu ni nzuri na tuna haakika tutalipa kisasi dhidi ya Toto hiyo Januari 28,” alisema Chale.

Chale aliongeza kua kwa matokeo ya mchezo wa jana (Januari 21,2012) kwa Villa kulala kwa goli 4-2, ni ya kawaida kwani nafasi bado hipo licha ya kuburuza mkia wa kubakia na pointi 7 zile zile.

“Kama munavyojua Villa tulimaliza mzunguko wa kwanza na pointi 7, yote yalichangiwa na hali mbaya ya ukata,migogoro ya hapa na pale sambamba na wachezaji kuhujumu timu ila kwa sasa tumejaribu kufaanya mabadiliko ikiwemo kusajiri wachezaji watano wapya kwa hakika tuna kila sababu ya kufanya vizuri kwa michezo iliyobaki” alisema Chale.

Aidha, kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo, Habib Kondo alikisifu kiwango cha timu yake licha ya kupoteza mchezo huo. Kondo alaisema watayasawadhisha makosa yote yaliyojitokjeza weakati wa mchezo huo ilikuwa washindani kwenye hatua hii ya lala salama.

“Kikosi change ndio kipya wengi wao ni wachezaji wachanga na hakika wengine ndio ilikua ni mara yao ya kwanza kucheza ligi kuu makosa yameonekana na nafasi wamezipaata wameshindwa kuzitumia basi nitayarekebisha kwenye mazoezi” aalimalizia Kondo.



Mwisho

No comments:

Post a Comment