Sunday, November 20, 2011

MAMA ASHA BILAL ALIPOKUWA MGENI RASMI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWA TAASISI YA ALLIANCE FRANCAISE TANZANIA!

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha wake wa Mabalozi wa Nchi za Afrika, Mama Juma Khalfan Mpango, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam Tanzania, iliyofanyika jana Novemba 17 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise Dar es Salaam. Kushoto ni Rahma Othman.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Asha Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam Tanzania, iliyofanyika jana Novemba 17 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini, Marcel Escure (kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Julia Giannetti.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza jambo na Balozi wa Ufaransa nchini, Marcel Escure, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam Tanzania, iliyofanyika jana Novemba 17 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise Dar es Salaam.
Mama Asha Bilal, akionyeshwa baadhi ya picha zilizokuwa katika ukumbi wa maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 Alliance Francaise.

No comments:

Post a Comment