Bendi ya Shule ya Sekondari Jitegemee ikitoa burudani mbele ya wageni waalikwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mwenyeji wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou.
Waziri Membe akipokea heshima kwa kupigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Attention Mbelez tembea......Visafisha njia.
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe, akihutubia katika sherehe za kilelel cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na miaka 66 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Membe aliishukuru UN kwa msaada mkubwa inaoupatia Tanzania kupitia wakala wake wa maendeleo na kusisitiza kuendeleza mema yote na kutatua changamoto zinazoikabili nchini hususani katika ongezeko la watu Duniani ambalo linatarajiwa kufikia Bilioni 7 mwaka huu na uwepo wa changamoto nyingi na nafasi mbalimbali.
Wawakilishi kutoka Balozi mbalimbali na viongozi wa Serikali wakifuatilia sherehe hizo zilizokuwa zikendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu ni Afisa Habari wa UN Information Centre Usia Ledama akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Mahadhi Juma aliyefuatana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou (katikati) alipotembelea banda la UN katika wiki ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru sambamba na 66 ya UN.
Pichani Juu timu ya Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini katika masuala ya Mawasiliano na Mahusiano wakijadiliana katika mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Pichani Juu kutoka kulia Sala Patterson – UN Communication Specialist, Usia Ledama na Hoyce Temu.(Picha zote na http://dewjiblog.com/).
No comments:
Post a Comment