Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Kulia) akiteta jambo na Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi Mwamvita Makamba kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kuwawezesha na Kuwajengea Uwezo wajasiriamali wadogo wanawake MWEI utakaowezeshwa na huduma ya M Pesa uliofanyika mwishoni mwa wiki kijiji cha Bwigiri mkoani Dodoma. Mpaka kufikia Julai 2011 tayari wanawake 4500 wamefikiwa na kukopeshwa shilingi milioni 90/-.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwaonesha baadhi ya wajasiriamali wadogo wanawake nembo ya mradi Kuwawezesha na Kuwajengea Uwezo wajasiriamali wadogo wanawake MWEI ulioanzishwa na Vodacom Tanzania ili kuwapa mikopo isiyo na riba mara baada ya kuuzindua mwishoni mwa wiki kwenye kijiji cha Bwigiri mkoani Dodoma.Wanaoshudia (Katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare na Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifafanuliwa jambo na mmoja ya wajasiriamali wadogo wa kijiji cha Bwigiri mkoani Dodoma alipokwenda kuzindua mradi wa Kuwawezesha na Kuwajengea Uwezo wajasiriamali wadogo wanawake MWEI utakaowezeshwa na huduma ya M Pesa kwa kutoa mikopo isiyo na riba mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare.
Waziri Mkuu Mizengo Pinga akiagana na mmoja wa wajasiriamali wadogo wanawake wa kijiji cha Bwigiri Mkoani Dodoma ambao wamepewa mikopo isiyo na riba kupitia mradi wa Kuwawezesha na Kuwajengea Uwezo wajasiriamali wadogo wanawake MWEI utakaowezeshwa na huduma ya M Pesa mara baada ya kuuzindua mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare.
Kikundi cha sanaa cha wanawake wa Kijiji cha Bwigiri mkoani Dodoma kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kuwawezesha na Kuwajengea Uwezo wajasiriamali wadogo wanawake MWEI utakaowezeshwa na huduma ya M Pesa inayotolewa na Vodacom uliofanywa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Mpaka kufikia Julai 2011 tayari wanawake 4500 wamefikiwa na kukopeshwa shilingi milioni 90/-.
No comments:
Post a Comment