Tuesday, July 26, 2011

SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA MATAWI YA BENKI ZA KILIMO!

Serikali imeombwa kuongeza matawi ya benki za kilimo nchini kufikia katika ngazi za mikoa na kanda ili kuwawezesha wakulima kufaidika na fedha zinazotolewa na Benki ya Rasilimali nchini (TIB) kwa malengo ya kuinua kilimo nchini.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) MUNDE ABDALLAH ameliambia Bunge mjini Dodoma kwamba kukosekana kwa matawi hayo kunachangia fedha hizo kuliwa na wajanja badala ya kuwafikia wakulima hususani wale wa vijijini.


Katika hatua nyingine Mheshimiwa MUNDE ametumia fursa hiyo kuikumbusha serikali kupeleka chakula cha msaada kwenye eneo la Tabora Manispaa lililoathiriwa na janga la mvua ili kuwaepusha wakazi wake na uhaba wa chakula.

No comments:

Post a Comment