Sunday, July 10, 2011

KIJIJI CHA NYANDEKWA CHAOMBA KIINGIZWE KWENYE MAENEO YA UTALII!

Wakazi wa kijiji cha Nyandekwa, mkoani Shinyanga wameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kukitambua kijiji hicho kuwa miongoni mwa vivutio vya kitalii nchini kufuatia kuwepo kwa jiwe linaloonyesha alama za unyayo wa mtemi maarufu kutoka kabila la wanyamwezi MWANAMARUNDE zaidi ya mika mia moja iliyopita.

Akizungumzia jiwe hilo mmoja wa Wakazi wa Kikijiji hicho HAMIS MANYANDA, amesema jiwe hilo kuwa pia lina asili ya mchezo wa bao na mashimo ambayo yalitumika kusagia nafaka ambapo alama zote hizo zipo wazi lakini hakuna jitihada zozote zilizofanyika za kulitunza jiwe hilo na Wizara husika.


MANYANDA amesema ikiwa wizara itatangaza jiwe hilo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watafika katika kijiji hicho kujionea na kujifunza mambo mengi kutokana na kumbukumbu hizo za kihistoria.

No comments:

Post a Comment