Tuesday, June 14, 2011

WIZARA YA ELIMU YAWATAKA WANACHUO UDOM KURUDI MADARASANI!

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Dakta Shukuru Kawambwa amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kurudi madarasani huku Serikali ikifanya utaratibu kwa wanafunzi hao kufanya mafunzo kwa vitendo katika mwaka huu wa fedha wa 2010/2011.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Dodoma kufuatia mgomo na maandamano waliofanya wanafunzi wa chuo hicho vitivo vya Sanaa na Sayansi ya Jamii, Sayansi Asilia pamoja na Hisabati Waziri Kawambwa amesema suala hilo limeshapatiwa ufumbuzi hivyo hakuna sababu ya wanafunzi hao kuendele na mgomo wa kutoingia madarasani.
Amesema kwa kuona umuhimu wa mafunzo kwa vitendo Serikali imeamua kuwa na Mpango wa mpito ambao utawezesha wanafunzi wa skuli hizo mbili katika Programu 13 kufanya mafunzo kwa vitendo kwa Mwaka wa masomo 2010/2011.
Amesema kuwa Fedha za mkopo kwa ajili ya Mafunzo hayo zitatolewa kabla ya kuanza kwa mafunzo husika na kwamba utaratibu huo utatoa fursa kwa Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) kutafiti kwa kina na kubaini umuhimu wa mafunzo kwa vitendo katika programu hizo 13.

No comments:

Post a Comment