Monday, June 6, 2011

SERIKALI YATAKA JAMII ISHIRIKI KAMPENI KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA, SOPHIA SIMBA na wadau wengine wakizindua mpango huo leo hii.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA akipanda kwenye moja ya pikipiki itakayotumika kwenye vituo vya afya wakati wa utekelezaji wa mpango huo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA akiwa na baadhi ya wanafunzi walioshiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuzuia vifo kwa watoto na akina mama wajawazito.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA, ameitaka jamii kushiriki katika kampeni ya kupunguza vifo vya Wanawake wajawazito na Watoto nchini, kufuatia asilimia 28 ya vifo vya wanawake kusababishwa na kutokwa damu nyingi wakati kujifungua.



Akizindua Kampeni hiyo, Waziri MPONDA, amesema tafiti za mwaka 2010 zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la Wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 47 hadi 50 na kwamba mpaka sasa zahanati 478 na vituo vya afya 78 vimejengwa nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, SOFIA SIMBA, amesema Serikali imeongeza kiwango cha udahili wa wanafunzi vyuoni kwa lengo la kupunguza tatizo la uhaba wa madaktari kwenye vituo mbalimbali vya Afya nchini.

No comments:

Post a Comment