Mbunge wa Mvomero AMOS MAKALLA amemuomba Waziri Mkuu MIZENGO PINDA kuingilia kati mgogoro wa kimaslahi baina yake na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, FATMA MWASSA ambaye amesitisha kugawa chakula cha maafa kwa wananchi waliokumbwa na maafa wilayani humo.
Akichangia makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu jana Bungeni Mjini Dodoma Mbunge MAKALA amesema kitendo kinachofanywa na Mkuu huyo wa wilaya yak Mvomero kutokana na masuala ya kisiasa ni sawa na kuwakomoa wahanga hao wa mafuriko ambao mpaka sasa wanahitaji chakula hicho.
Akisoma makadirio ya Wizara yak Ofisi yake Waziri Mkuu PINDA amesema sekta bBinafsi ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa taifa na kwa kuzingatia hilo itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji kwa lengo la kuendeleza sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment