Mitambo ya kuzalisha umeme ya SONGAS
Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuanza kwa mgao wa umeme, ambao kwa mujibu wa shirika la umeme nchini Tanesco, mgao huo unatokana na upungufu mkubwa katika gridi ya taifa , baadhi wa wakazi jijini Dar es Salaam wameuzungumzia mgao huo na kuhoji suala hilo kutopatiwa ufumbuzi wa kudumu kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme nchini Mhandisi William Mhando alinukuliwa katika tangazo hilo akisema, mgao huo unatokana na kusimamishwa kwa uzalishaji wa gesi asili iliyopo katika kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi , kwa lengo la kuruhusu wamiliki wa visima hivyo kuvifanyia ukaguzi na ukarabati kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa gesi ya kufulia umeme.
Mgao huo utakaonza Mei 19, utainyima nchi umeme kwa saa 16 katika kipindi cha saa 24 kila siku.
No comments:
Post a Comment