BI HILDA BANDIO (Katikati)
ROSE CHACHA MARWA akionesha moja ya mavavi ya ubunifu yatakayooneshwa
Watanzania watafaidika na maliasili zilizopo katika maeneo yao ikiwa serikali itaweka kipaumbele katika kufikisha elimu ya ujasiliamali hasa ule wa kutumia vitu vya asili katika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama nguo na mapambo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Tanzania MMAWATA BI HILDA BANDIO amesema kama jamii itaelimishwa kutumia vitu vya asili wataweza kujikomboa kimaisha kwani vifaa vyake vinalimwa au kuzalishwa hata na wakulima wadogo.
Kwa kushirikiana na ubalozi wa USWIZI asasi ya MMAWATA itafanya onesho la mavazi ya asili kwa lengo la kuhamasisha jamii kuanza kutumia vitu vya asili katika kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment