

Wasanii chipukizi walioshiriki shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,kutoka kulia ni Pacha Great akimchana live kwa kughani msanii mwenzie aitwaye Chalz Gibson wakati wa shindano hilo,ambpo Pacha aliibuka mshindi na kuwa mshindi wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 ndani ya jiji la Arusha.

Mmoja wa majaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa, Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali akifafanua jambo kwa washabiki na watazamaji mbalimbali waliofika kwenye shindano hilo ndani ya ukumbi wa Mawingu Club,mjini Arusha mapema leo jioni.



Mwanadada mwingine aliyejitokeza kunogesha shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,aliyejulikana kwa jina la Catrina akiimba kwa sauti tamu kabisa na yenye kusisimua mashabiki jioni ya leo ndani ya Mawingu Club,jijini Arusha.

Msanii mahiri wa hip hop kwa jiji la Arusha atambulikae kwa jina la kisanii,JCB akiwarusha washabiki wa muziki wa hip hop,jioni ya leo ndani ya ukumbi wa Mawingu Club,wakati wa kumsaka kinara wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa.

Mratibu wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,Adam Mchiomvu akitajana majina yaliyoingia fainali kwenye shindano hilo,ambalo limekuwa na msisimko mkubwa kwa vijana wengi wa jiji la Arusha,katika mchakato mzima wa shindano hilo walijitokeza vijana 32,wakachunjwa na kupatikana wengine 12,na hatimaye kuwapata sita ambao walishindana vikali,aidha katika sita hao aliihitajika kinara mmoja tu wa kughani kwa miondoko huru.

Mwanadada machachari kabisa aitwaye Tiger Eyes akionesha umahiri wake wa kughani mbele mashabiki waliofika kwenye shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa.

No comments:
Post a Comment