Kutokana na kuwepo kwa tatizo la ajira nchini hasa kwa vijana hivi karibuni Waziri Mkuu Mstaafu EDWARD LOWASA alinukuliwa na vyombo vya habari akisema tatizo hilo ni Bomu linalosubiri kulipuka.
Kutokana na hali hiyo Serikali imetoa ufafanuzi na kubainisha kuwa ukosefu wa ajira nchini umepungua kutoka asilimia 12.9 na kufikia asilimia 11.6 huku tatizo kubwa likiwemo mijini ambapo Dar es Salaam ukosefu wa ajira ni asilimia 31.5 wakati maeneo ya vijijini tatizo hilo lipo kwa asilimia 7.5.
Waziri wa Kazi na Ajira GAUDENSIA KABAKA amesema Serikali imekuwa ikijitahidi kuzalisha ajira kwa kufungua milango kwa wazwekezaji na kuwawekea wananchi mazingira rafiki ambapo kwa mwaka zimekuwa zikizalisha ajira kati ya laki nane na milioni moja na kubainisha kuwa tatizo la ajira ni tatizo la Dunia nzima.
No comments:
Post a Comment