Tuesday, February 21, 2012

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAHAIRISHA KUPANGA TAREHE YA KUSIKILIZA KESI YA DAVID KAFULILA NA WENZAKE!

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha kutaja tarehe rasmi ya kuanza kusikiliza shauri la Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR Mageuzi DAVID KAFULILA na wajumbe wenzake watano wa Halmashauri kuu ya chama hicho taifa dhidi ya NCCR Mageuzi wakipinga kukiukwa kwa taratibu za kuwafukuza uanachama.



Akiahirisha kesi hiyo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Jaji AMIR MSUMI amesema Jaji ALIS CHUNGUWILE anayepaswa kupanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo yuko nje ya mkoa kikazi na anatarajiwa kuwepo Jijini Dar es Salaam Machi 15 mwaka huu.


Akizungumzia suala hilo KAFULILA amesema ni matarajio yake jambo hilo halitaathiri mwenendo wa kesi hiyo na kwamba misingi ya sheria itafuatwa na hatimaye haki kutendeka kwa pande zote. Desemba 26 mwaka jana Mahakama Kuu ilizuia utekelezaji wa uamuzi wa chama cha NCCR Mageuzi kumvua uanachama KAFULILA na wenzake kwa tuhuma za kutoa siri za chama.

No comments:

Post a Comment