Tuesday, January 17, 2012

TANZANIA RED CROSS 'ACTION TEAM' WAENDELEA NA UJENZI MABWEPANDE!


Mratibu wa Ujenzi wa nyumba za muda za waathirika wa mafuriko, Aidan David Mwalyambwile (kulia) wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Red Cross), akiwapatia maelezo vijana wa kikosi cha maafa na uokoaji mkoa wa Dar es Salaam (Action team) namna ya kujenga nyumba hizo katika viwanja vya Mabwepande jijini Dar es Salaam, mwishoni mwaka wiki, mpaka sasa nyumba zaidi ya 200 zimeshajengwa chini ya Msalaba Mwekundu. (Picha na Andrew Chale).
TRC's Action team, wakiwa katika ujenzi wa nyumba hizo za muda katika viwanja vya Mabwepande.


Na Andrew ChaleUjenzi wa makazi ya muda huko Mabwepande unaendelea kwa takribani wiki ya pili sasa ambao unafanywa na kikosi maalum cha Maafa na Uokoaji mkoa wa Dar es Salaam (Action Team) cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Red Cross), ambapo muda wowote kuanzia sasa kaya 300 zitapelekwa huko kwa ajili ya kuanza maisha mapya sambamba na kujenga nyumba zao za kudumu.
Viwanja hivyo kwa ajiri ya waathirika wa mafuriko jijini Dar es Salaam, vipo nje ya jiji la Dar Kilometa 6 kutoka njia panda ya Bunju B, mpaka kufika huko Mabwepande huku usafiri wake mkubwa ukiwa ni pikipiki kwa nauli ya shilingi 1500/2000, huku kwa taxbubu nauli ikiwa ni bukubuku kwa abiria wanne.

Mpaka sasa tayari kikosi hicho maalufu kama 'TRC's Action Team', kimeweza kufikisha nyumba za muda zaidi ya 200 na tayari Rais Jakaya Kikwete ameweza kujitembelea na kujionea hali halisi ya utendaji wa kazi wa kikosi hicho ambacho pia kinashirikiana na jeshi la kujenga Taifa 'JKT'.

Katika ujenzi huo unaosimamiwa na mtaalamu maalum wa TRC's, Aidan David, alisema kua nyumba hizo ni imara na zinauwezo mkubwa wa kukaa familia tano kwa kila moja na zinadumu iwapo mtumiaji ataitumia kwa ukamilifu mkubwa sambamba na kuifanyia marekebisho kidogo.

Aidan alisema kua, watahakikisha wanajenga nyumba zaidi ya 300 katika viwanja hivyo na zitakua faraja kwa wakazi watakaoletwa hapo na watazitumia huku wakiendelea na ujenzi wa nyumba zao za kudumu.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi alibaini kasoro mbalimbali ikiwemo ufinyu wa upatikanaji huduma muhimu ikiwemo za maduka na vyakula huku vyakula vilivyopo vikiwa havikidhi mahitaji halisi ya walaji wanaofika kila kukicha katika maeneo ya viwanja hivyo kwa sasa.

Hivyo wafanyabiashara wa makampuni ikiwemo ya simu,vinywaji na chakula wanashahuriwa kufika eneo hilo la viwanja hivyo ilikurahisisha tatizo la ukosefu wa mahitaji muhimu ambapo kwa siku Mabwepande kwenye mradi huo wa viwanja inapokea watu zaidi ya 100 mbali ya wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu,askari wa JKT, wataalamu wa barabara na Wakandarasi wanaofanya savei na kupima viwanja hivyo.

Onyo epuka matapeli tayari wameshavamia kwenye viwanja hivyo na namba za nyumba za watu wa jangwani wakidai kua viwanja hivyo wakipewa watawauzia watu hivyo uchunguzi umebaini watu wengi wanamiminika huko wakiangalia mianya ya kufanikisha hadhima hiyo ikiwemo kuwahadaa maafisa ardhi wa Kinondoni na kamati ya maafa ya waziri mkuu. Mwandishi ni Mjumbe wa kikosi cha maafa na uokoaji cha msalaba mwekundu Tanzania).

No comments:

Post a Comment