Tuesday, December 20, 2011

ZAIDI YA ASILIMIA 60 YA KESI ZILIZOSUGHULIKIWA NA WILAC ZINAHUSU NDOA NA FAMILIA!

Zaidi ya asilimia 60 ya kesi zilizoshughulikiwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake na watoto (WILAC) kwa kipindi cha mwezi April na Juni mwaka huu zinahusu ndoa na familia.

Mwanasheria, Wakili na Meneja mafunzo wa WILAC THEODOSIA MUHULO amesema katika kipindi hicho kulikuwa na kesi 549 kati yake kesi 177 zikihusiana na masuala ya ndoa na familia ambapo mwisho wa kesi hizo huwa ni kuvunjika kwa ndoa na mgawanyo wa mali.


Takwimu za kituo hiki pia zinaonesha kuwa wawazi wengi ambao watoto wao wamebakwa huamua kusameheana na watuhumiwa au fomu namba tatu kwa ajili ya matibabu kujazwa na Madaktari zikionyesha hakuna ubakaji uliofanywa na hivyo wazazi kukata tamaa ya kuendelea na kesi hizo.

No comments:

Post a Comment