Wednesday, December 21, 2011

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DSM ZAUA WATU 13!

Na Theeastafrica Bloger
Mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar es Salaam zimendelea kuleta maafa makubwa ikiwemo kusababisha vifo vya takribani watu watano na kuharibu miundombinu ya barabara ikiwemo kumeguka kwa daraja la Mbezi linalounganisha barabara ya Bagamoyo kati ya Mbezi Beach na Kawe.

Kituo hiki kimeshuhudia mawimbi makubwa ya maji yakimomonyoa daraja la mto Mbezi hali iliyosababisha Jeshi la Polisi kuzuia magari kupita juu ya daraja hilo likihofia usalama wa watuamiaji wa barabara hiyo.


Katika eneo la Tabata Matumbi kwenye bonde la mto Msimbazi hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya maji yaliyokuwa yakitokea Tabata Kinyerezi na vitongoji vyake kusomba watu, nyumba na mali zao na hatimaye kusababisha vifo vya watu watatu na mifugo yao.


Mmoja ya wahanga wa mvua hizo Bw SHARRIF RAJAB ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea alisombwa na maji na kwa msaada wa ng’ombe wake aliweza kufika hadi katika daraja la matumbi ambako alikaa juu ya mti kwa zaidi ya saa tatu hadi alipookolewa na wasamaria wema.


Kabla ya kuokolewa helkopta ya Jeshi la Polisi ilipita katika eneo hilo bila kutoa msaada wowote kwa muahanga huyo na wengine waliokuwa juu ya vichwa vya magari hadi wasamaria wema walipojitosa kwa kutumia kamba kwenda kumuokoa Bw RAJAB.


Kwenye bonde la Kigogo na eneo la Jangwani, kituo hiki kimeshuhudia maji yakikatiza juu ya daraja la Jangwani hali iliyosababisha kukatishwa kwa mawasiliano baina ya upande wa Kariakoo na Magomeni.


Bonde la Mkwajuni Kinondoni maafa hayakuwaacha salama wakazi waliojenga mabondeni, kwani mafuriko kutokana na mvua hizo yalizingira nyumba zote la eneo hilo na baadhi ya wanafamilia walijitahidi kuokoa baadhi ya mali ikiwemo mifugo yao.

No comments:

Post a Comment