Wednesday, October 5, 2011

VODACOM YADHAMINI MASHINDANO YA UVUVI KISIWANI SINDA!

Wafanyakazi wa boti ya Mistress wakiwa wamebeba samaki zilizovuliwa katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi yajulikanayo kama Latham Open yaliyoshirikisha nchi sita na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Kikundi cha Sanaa cha Jambo brothers kutoka Zanzibar kikionyesha sarakasi mbalimbali katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyokuwa yakiendelea kisiwani humo, ambayo pia yalidhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club jijni Dar es Salaam (kushoto) akitoa neon la shukrani kwa wadhamini wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda hivi karibuni ambao ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, (kulia) Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akitoa zawadi kwa mshindi wa uvuvi kwa upande wa watoto Kyle Balarin (15) aliyekuwa akitumia boti ya Tarka katika mashindano yaliyofanyika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club akishuhudia utoaji wa zawadi hizo.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akimkabidhi zawadi Alfred Charles kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa upande wa boti ya Mistress katika mashindano yaliyofanyika huko Sinda kisiwani mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Washindi wa mashindano ya uvuvi ya Latham Open wakifurahia tuzo zao za ushindi mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika Kisiwani Sinda mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mwanamuziki Mark Hart kutoka Afrika Kusini akitumbuiza katika mashindano ya uvuvi yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, mashindano hayo yaliyoshirikisha nchi sita yalidhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment