Monday, October 24, 2011

MAONYESHO YA MCHEZO WA KAPOEIRA @ RUSSIAN CULTURAL CENTRE!

Makamu wa Balozi wa Brazil nchini Mhe. Ronaldo Vieira akiwakaribisha wageni katika Maonyesho ya Mchezo wa Kapoeira yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia.

Mhe. Ronaldo amesema kwa mara ya Kwanza mchezo wa Kapoeira ulizinduliwa nchini Tanzania Mwezi June mwaka jana na kwa jijini Dar es Salaam mafunzo ya mchezo huo yanafanyika katika kituo cha Fitness Centre Msasani jijini Dar es Salaam na kuwakaribisha Wakazi wote wa jijini kuhudhuria mafunzo ya Mchezo huo.
Mwalimu wa Mchezo wa Kapoeira ambao ni utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil Mestra Janja akizungumzia umuhimu na faida za mchezo huo kwa wageni waliohudhuria Onyesho la mchezo huo katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kapoelista Gabriel Limaverde ambaye alikuwa akitafsiri Ujumbe huo kwa Lugha ya Kingereza.


Mestra Janja amefafanua kwamba Kapoeira ni Utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil na Alama madhubuti ya Wabrazil, hazina Muhimu ya Utamaduni wa Utu na Umoja na ni Sanaa ya Kibrazil ya Ulinzi na Kujikomboa kutumia akili na viungo vya kibinadamu. Pia ni sehemu ya taaluma, fani na ujenzi maalum nchini Brazil na nchi zingine ambako imekubalika na kutambulika, hivyo inafundishwa na inachezwa katika nyanja mbalimbali na kuzingatiwa katika tafiti za viwango tofauti vikijumuisha na vya Shahada ya Uzamili (Master's Digrii) na Digrii ya Udaktari wa Falsafa kwenye masomo ya Anthropologia, Historia, Soshologia, Elimu na Elimu ya Viungo.
                     Wadau wakifuatilia kwa umakini Historia ya mchezo huo kutoka kwa Mestra Janja.
                                                            Wadau wakifuatilia kwa umakini.
                                                Picha za Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Makamu wa Balozi wa Brazil nchini Mhe. Ronaldo Vieira katika picha ya pamoja na Mwalimu Janja pamoja na Makapoelista.

No comments:

Post a Comment