Monday, October 31, 2011

ATCL KUANZA KUTOA HUDUMA KUELEKEA KIGOMA NA MWANZA!

Serikali imesema wakati Shirika la Ndege la TANZANIA (ATCL), likitarajiwa kuanza kutoa huduma ya usafiri siku ya kesho haitarajii kuona tena shirika hilo likiomba kuwezeshwa kimtaji kuendelea kutoa huduma zake.

Akizungumza katika mkutano wa mpango wa mwaka wa sekta ya miundombinu, Jijini Dar es salaam, Waziri wa Uchukuzi OMARI NUNDU, amesema pamoja na kuliwezesha shirika hilo, itaendelea na juhudi za kuboresha zaidi miundombinu ikiwemo kuongeza idadi ya bandari na kuziboresha zaidi zile za Dar es salaam, Mtwara na Tanga.


Katika hatua nyingime Waziri NUNDU, ameeleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya miundombinu katika miaka 50 ya uhuru ikiwemo ujenzi wa barabara, bandari pamoja na usafiri wa anga hayapaswi kusibezwe.
Hii ni aina ya ndege ambayo itaanza kutoa huduma kesho kuelekea mikoa ya Mtwara, Kigoma na Mwanza.

No comments:

Post a Comment