Wednesday, September 21, 2011

SHEAR ILLUSION KUKUSANYA MILIONI 50 KUSAIDIA HOSPITALI ZA CCBRT NA AMANA!

Kiasi cha shilingi Milioni 50 kinahitajika katika kutunisha mfuko utakaosaidia akina mama wenye matatizo ya fistula katika Hospitali ya CCBRT na kuwezesha ukarabati wa mfumo mzima wa maji safi na maji taka katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na kituo hiki Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mfuko wa Shear Charity Ball, SHEKHA NASSER amesema fedha hizo zitasaidia kuongeza kiwango cha huduma za tiba zinazotolewa kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kujenga mwamko wa jamii kusaidiana.

No comments:

Post a Comment