Wednesday, July 6, 2011

VURUGU ZAZUKA MANZESE TIP TOP NA MTAA WA MAKOROBOI JIJINI MWANZA!

Vurugu zazuka Manzese TIP TOP, vijana wazuia mwili wa mwenzao usizikwe.

Na Eastafrica Blog
Vurugu zimetawala katika eneo la Manzese Tip Top jijini Dar es Salam baada ya vijana wa mtaa huo kukataa mwili wa mwenzao aliyefariki ghafla usizikwe kwa madai kwa kijana huyo hajafa. Taarifa kutoka ndani ya eneo hilo zinadai kwamba baada ya kijana huyo kufa watu saba walipandisha mashetani kwamba kijana huyo hajafa na kwamba amechukuliwa katika mazingira ya kutatanisha hivyo anaweza kufufuka kama waganga wa kienyeji watajitokeza.


Hivyo kwa kuwa baba wa marehemu anapinga imani za kishirikina aliamuru ndugu wa marehemu wachimbe kaburi kwa ajili ya mazishi leo jambo ambalo limeshindikana. Kwani vijana hao wanasema kama watu saba wamepandisha mashetani basi kuna ukweli wa jambo hilo kwamba marehemu huyo amekufa katika mazingira ya kishirikina na hivyo wanataka afufuliwe ili andelee na maisha yake kama awali.


Mzozo huo unapelekea Polisi kufika katika eneo hilo ili kuruhusu shughuli za mazishi ziendelee lakini hali bado inakuwa tata kwani vijana hao ambao wanawazidi Polisi kwa idadi wanafanikiwa kuwazidi nguvu polisi na kuwashurutisha kutoondoka na mwili wa marehemu huyo kuupeleka hospitali.


Sakata hilo linasababisha polisi kuzungumza na baba wa marehemu anayekubali mwili wa mwanae ukahifadhiwe Hospitali kuruhusu mazungumzo kati ya vijana hao na ndugu wa marehemu. Hata hivyo askari hao wanapojaribu kutoka na mwili wa marehemu vijana hao wanawazuia na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za mto kuondoka na mwili wa marehemu.


Kweli wanafanikiwa lakini kinachooendelea nyuma yake ni vijana hao kwenda kuchoma kituo kidogo cha Polisi kwa madai kwamba askari hao wamechangia kutoa taarifa za tukio hilo ili mwili huo uzikwe.

Lakini wakati hayo yakitokea Jijini Dar es Salaam Taarifa zilizotufikia kutoka Jijini Mwanza zinaeleza kwamba kumezuka vurugu kubwa kati ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga na Polisi jijini humo. Tukio hilo limetokea baada ya wafanyabiashara hao kukaidi kuondoka eneo la msikiti mtaa wa Makoroboi kwa madai kwamba jeshi la Polisi linakiuka makubaliano waliojiwekea kati yao na Halmashauri ya jiji la Mwanza.


Huyu hapa ni Mwakilishi wa Clouds FM jijini Mwanza G SENGO aliyopo eneo la tukio akielezea hali halisi ya vurugu hizo ambazo zinadaiwa kusababisha vifo na majeruhi kadhaa wakati polisi wakijaribu kuwatawanya wafanyabiashara hao. Kwa taarifa zaidi za matukio hayo tembelea hapahapa www.theeastafrica.blogspot.com kwa uelewa!

No comments:

Post a Comment