Monday, June 27, 2011

CHAMA CHA USHIRIKA NA UMWAGILIAJI CHAURU KUONGEZA MAVUNO!

Chama cha ushirika wa kilimo cha umwagiliaji Ruvu CHAURU wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani kinatarajia ongezeko la mavuno kati ya tani 600 hadi 700 katika mwaka huu wa 2011/2012. Mwenyekiti wa ushirika huo, BW. ZAHOR SENG'ENGE amesema sababu kubwa ya kuongezeka kwa mavuno mwaka huu ni hali ya hewa nzuri iliyojitokeza ikichangiwa na uwepo wa mvua za kutosha.

Hadi sasa baadhi ya wakulima wamekwishaanza kuvuna mpunga na wanatarajia kuvuna katika awamu tatu ambapo awamu ya pili itaanza JUNI 30 na ya tatu itakuwa kati ya Septemba na Oktoba. Bwana SENG’ENG’E ameongeza kuwa ushirika kupitia CHAURU wanachama wamekuwa wakilimiwa hekari kwa shilingi 35,000, kusawazisha udongo shiling 20,000/- viwango hivyo ambavyo ni nje ya soko huria jambo linalotoa unafuu kwa mkulima kupata huduma hizo.

No comments:

Post a Comment