Thursday, May 3, 2012

WAKUU WA TAASISI ZA UMOJA WA MATAIFA (UN) WAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk Alberic Kacou (kushoto), leo akihutubia Jukwaa la Wahariri aliwashakuru wahariri nchini kwa kazi kubwa wanayofanya katika utoaji wa taarifa za umoja huo. Amesema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari.
 
 Mkurugenzi wa UNAIDS Tanzania Dr. Luc Barrier (kushoto) amefafanua kwamba mapambano yatayoweza kuzaa matunda dhidi ya UKIMWI katika nchi ni yale ambayo yatahusisha sekta zote za jamii. Alisistiza kwamba kaasisi taasis iliyopo chini ya Umoja wa Mataifa, shughuli zao zinaendeshwa sambamba na sera za nchi husika katika masuala ya kupambana na UKIMWI.

 Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot alisema Pamoja na utajiri mkubwa wa maliasili, Poimsot amesema kwamba Tanzania bado ina wananchi wengi sana ambao ni maskini. Amefafanua kwamba pamoja na pato la taifa limekuwa likiongeza kuanzia mwaka 2000, hali hiyo imekuwa ikitokea katika sekta ambazo haziongezi ajira kwa wananchi wa kawaida.

Msaidizi Mshauri wa Umoja wa Mataifa Bw. Tobias Rahm akijumuisha katika mkutano wa taasisi za Umoja wa Mataifa na Jukwaa la Wahariri, Rahm alisema kwamba ni matumaini yake kuwa vyombo vya habari vitaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi katika kuongea ufanisi na uelewa wa shughuli zao.

No comments:

Post a Comment