Monday, May 28, 2012

HALMASHAURI YA NJOMBE YAKABIDIWA MITAMBO YA KUTENGENEZERA BARABARA

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya GF Trucks & Equipments leo imekabidhi mitambo ya kutengenezea barabara kwa halmashauri ya Njombe katika hafla iliyofanyika jijini Da es Salaam

 

Akiongea wakati wa hafla hiyo afisa masoko mwandamizi wa kampuni hiyo Eng Juma Hamsini alisema halmashauri ya Njombe imekuwa ya kwanza kuitikia wito uliotolewa na kampuni hiyo wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT).ya kuzitaka halmashauri za Miji na serikali za mitaa kuchangamkia ofa ya punguzo na ukopeshwaji wa mitambo na magari makubwa aina ya Tiper (FAW) katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miji yao kwa gharama nafuu.

Alisema Njombe walikuja na tukazungumza nao kupitia benki ya CRDB tulikubaliana nao kuwapatia mashine tatu Motor Greda, Vibration Roll na Extraverte ambazo zote zina thamani ya shilling million 716 na malipo ya awali yakiwa ni shilingi 266 na million 450 watamalizia kwa kipindi cha miezi 12

 

Aidha Hamsin alisisitiza kuwa faida kubwa ambazo Halmashauri za miji itazipata ni pale watakapo toa tenda kwa mkandarasi aliyeshinda atalazimika kukodisha mitambo ya halmashauri ambayo inatoka kwao.

 

Alisema kampuni yake inataka ushirikiano huu uwe na maana baada ya Halmashauri na miji kununua magari na mitambo ya kukodisha na hizo mamlaka kuwakodisha makandarasi wanaoshinda tenda mbalimbali hapa nchini.

 

Aliongeza kwamba Gf wanautaratibu wa kukopesha vitendea kazi kwa wakandarasi wa kizalendo pindi wanaposhinda tenda ya kujenga au kutengeneza barabara katika miji ya Tanzania .
Hamsini alisema kwamba ndani ya kampuni yao wana mikopo ya aina mbili moja ni kati ya kampuni na mteja na nyingine ni kati ya kampuni na mashirika ya serikali kama vile halmashauri,manispaa, wizara na taasisi mbalimbali za serikali.

Afisa Masoko alitanabahisha kwamba mikopo ya ndani kati yao na watu binafsi mteja analazimika kulipa asilimia 50 ya gharama ya gari au kifaa na asilimia 50 inayobaki atatakiwa kulipa ndani ya miezi 6 .
Hamis alifafanua kwamba kwa wateja na watu binafsi ambao hawawezi kukidhi vigezo vya aina ya mikopo miwili hiyo wanaweza kutumia benki ya Stabic na KCB kwa kulipa asilimia 20 tu na asilimia 80 kudhaminiwa na benki husika.

Kwa upande wa serikali na taasisi zake wanatakiwa kulipa asilimia 30 na asilimia inayobaki watatakiwa kulipa ndani ya miezi 12 na kumaliza mkopo mzima.Vilevile baadhi halmashauri ambazo wamenufaika na mpango huo kwa kukopeshwa ni Ilala ,Tanga , Kigoma Ujiji na Mbeya alimaliza Hamsini na kuzitaka halmashauri nyingine kuga mfano huu.

No comments:

Post a Comment