Monday, September 12, 2011

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGANA NA MABALOZI WA VATICAN NA JAPAN, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Joseph Chennoth, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Septemba 9, 2011 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Balozi Chennoth amekaa nchini miaka sita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Joseph Chennoth, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2011 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Hiroshi Nakagawa, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Septemba 9, 2011 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Hiroshi Nakagawa, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Septemba 9, 2011 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AAGANA NA MABALOZI WA VATICAN NA JAPAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameagana na mabalozi wa Vatican na Japan ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 09, 2011.


Wa kwanza kufika katika ofisi ya Makamu wa Rais alikuwa Askofu Mkuu na Mwakilishi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Joseph Chennoth ambaye alianza kwa kusifu ukarimu wa watu wa Tanzania huku akifafanua kuwa hali hii ni matunda yatokanayo na msingi imara uliojengwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyeliwezesha taifa hili kuwa na utu na watu wake kumudu kuishi kwa ushirikiano bila kubaguana.

Balozi Chennot alimwambia Makamu wa Rais pia kuwa, tangu aingie nchini miaka sita iliyopita amefurahi kuona namna Kanisa Katoliki linavyoshirikiana na serikali katika huduma za jamii katika maeneo yote, huduma ambazo zinatolewa kwa wananchi wote.


Dkt. Bilal alimwambia Balozi Chennoth kuwa Tanzania inathamini sana mchango wa kanisa katika kuwaendeleza wananchi na kwamba uhusiano huu utadumu kwa kuwa unazingatia matakwa na mahitaji ya wananchi wote. Balozi Chennoth alimnukuu Papa Paul VI aliyewahi kusema; ‘maendeleo ni jina mbadala la amani’ na kueleza Tanzania aliyoikuta wakati anafika si hii iliyopo sasa kwa kuwa kuna amani inayoashiria maendeleo kwa wananchi. Akisisitiza katika hoja hii Makamu wa Rais alisema kuwa, sifa kubwa inabakia kwa Mwalimu Nyerere kwa kuwa alifanya kazi kubwa ambayo matunda yake tunayaona hata sasa.


Kwa upande wa Balozi wa Japan Hiroshi Nakagawa ambaye amekaa miaka miwili alimueleza Makamu wa Rais kuwa Japan inafurahi kuona namna Tanzania inavyoendesha mambo yake na akafafanua pia kuwa nchi hiyo itazidisha mchango wake katika shughuli za maendeleo nchini. Makamu wa Rais alimueleza Balozi Nakagawa kuwa, Tanzania inathamini sana ushirikiano na Japan na kisha akaongeza kuwa Tanzania inatambua kipindi ambacho Japan inapitia hasa sasa baada ya kukumbwa na janga la Tsunami ambalo limeifanya Japan nayo kutokuwa na umeme wa uhakika.


Balozi Nakagawa alimueleza Makamu wa Rais pia kuwa, Japan itazidi kuendeleza ushirikiano katika sekta za Kilimo, utoaji wa huduma za Maji kama ifanyikavyo mikoa ya Mara na Mtwara ambapo miradi hiyo itahamia mkoa wa Tabora mwakani. Tena nchi hiyo itazidi kushiriki katika miradi ya barabara sambamba na sekta ya nishati.

No comments:

Post a Comment