Monday, September 12, 2011

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA VITUO VYA UOKOAJI AJALI YA MELI YA NUNGWI ZANZIBAR!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji, leo Septemba 11, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua maeneo yaliyokuwa yakitumika kupokelea na kuhifadhi miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya Spice, pamoja na majeruhi waliokuwa wakipitishwa katika eneo hilo la Ufukwe wa Bahari ya Hindi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Septemba 11, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na kumpa pole mmoja kati ya wakazi wa Unguja waliopotelewa na ndugu katika ajali ya meli ya Spice iliyotokea eneo la Nungwi, wakati makamu alipotembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar jana Septemba 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Viwanja vya Maisala mjini Unguja, wakati alipotembelea katika eneo hilo lililokuwa likitumika kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice jana Septemba 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati walipokutana katika viwanja vya Maisala, walipofika kutembelea mabanda ya kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice jana Septemba 10. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment