Baadhi ya wanaume Mkoani Shinyanga wamedai kuwa suala la Serikali kwa kushirikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutumia muda mwingi kujadili sheria inayomkandamiza mwanamke huku wakisahau kumtaja mwanaume inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuleta mfumo jike.
Akizungumza kwenye mafunzo yaliondaliwa kujadili haki za msingi za mwananmke, Mtendaji wa Kata ya Lubaga DEOGRATUS MASALU amesema kuwa sheria hiyo inamtetea zaidi mwanamke na kumsahau mwanaume hivyo Serikali isipoangalia itaingia tena gharama ya kuzuia mfumo huo kwenye jamii.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Kivulini la mkoani Shinyanga linalotetea haki za wanawake ili kuijadili sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuwa ifanyiwe marekebisho kwa sababu inamkandamiza zaidi mwanamke.
No comments:
Post a Comment