Tuesday, September 27, 2011

HARAMBEE FEDHA ZA SHEAR ILLUSION YAPIGWA JEKI NA SBL KWA MILIONI 36!

Mkurugenzi wa Shear Illusion Shekha Nasser kulia akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika kwenye makano makuu ya kampuni ya Serengeti Breweriers jijini Dar es salaam anayefuatia katika picha ni Meneja Muhusiano na mawasiliano wa Serengeti Breweriers Nandi Mwiyombela na mwisho ni Imani Lwinga Meneja Mawasiliano (SBL).

Harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuzisaidia taasisi mbili za CCBRT na hospitari ya Amana za Jijini Dar es salaam imefiki jumla ya shilingi milioni 36 kufuatia Kampuni ya Serengeti kutangaza udhamini wenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa taasisi hizo.

Meneja Mahusiano ya Jamii wa Kampuni ya Serengeti Breweries NANDI MWIYOMBELA amesema kampuni hiyo imetangaza rasmi udhamini huo ili kutoa kipaumbele kwa huduma za kijamii.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shear Illusion, SHEKHA NASSER ambae ni mratibu wa zoezi hilo amesema fedha hizo zitatumika kwa Malengo yaliyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment