Thursday, August 25, 2011

AMREF TANZANIA YAOMBA JAMII IELIMISHWE KUHUSU SERA NA HAKI ZA VIJANA!

Jamii nchini ikielimishwa kuhusiana na sera na haki za vijana itasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana kuanzia umri wa miaka 10 hadi 24 katika kupata haki na afya ya uzazi katika maeneo yao.

Akizungumza kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na Shirika la Afya na Utafiti Afrika (AMREF) Tanzania kuhusiana na afya ya uzazi kwa vijana, Mratibu wa Afya ya Uzazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii DK ELIZABETH MAPELA amesema ukosefu wa elimu hiyo umechangia vijana kujiingiza kwenye ngono zembe bila kutarajia.


Kwa upande wake DK GRACE MAGEMBE ambaye alikuwa mtoa mada kuhusiana na mradi huo wa afya ya uzazi salama kwa vijana amesema vifo 454 hutokana na uzazi katika kila vizazi 100,000/-.

No comments:

Post a Comment