Monday, July 18, 2011

VITENDO VYA WANANCHI KUCHUKUA SHERIA MKONONI VYAONGEZEKA - LHRC.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema suala la kuchukua sheria mikononi nchini limekithiri kufuatia kubainika kuwa si wananchi pekee bali hata vyombo vya usalama vimekuwa vikivunja sheria kutokana na ukosefu wa utawala bora.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya miezi sita tangu January mwaka huu, Mtafiti kutoka Kituo hicho, ONESMO OLENGURUMWA, amesema katika utafiti uliofanywa na kituo hicho kwenye mikoa 9 nchini umeonyesha kuwa wananchi 22 na polisi watano wamepoteza maisha kutokana na wananchi pamoja na Jeshi la Polisi kujichukulia sheria mikononi.


Naye kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, IMELDA URIO, amesema vitendo vya uvunjifu wa sheria vinachangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ngumu ya maisha huku akiwataka wananchi pamoja na Serikali kuepukana na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment