Wednesday, August 17, 2011

VIJIJI VITANO BAGAMOYO KUNUFAIKA NA MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA!

Wakazi wa Vijiji vipatavyo vitano vilivyopo Bagamoyo mkoa wa pwani wanatazamiwa kufaidika na mradi wa uchimbaji visima vya maji safi na salama vipatavyo sita katika maeneo yao.

Mradi huo umepangwa kutekelezwa katika vijiji vya Pande, yombo, Mbuyuni, Madukani pamoja na Makunguni na utagharimu kiasi cha shilingi milioni 42.


Akizungumza jijini DSM mkurugenzi wa taasisi ya Afya ya Ifakara Dakta SALIM ABDALLAH amesema kukamilika kwa mradi wa Visima katika maeneo hayo kutasaidia upatikanaji wa maji safi na salama yaliyokusudiwa kwa lengo la kuendeleza na kulinda afya za wananchi wa Vijiji hivyo.


Fedha za mradi huo zimetokana na michango ya mbalimbali ya wahisani kutoka Sekta Binafsi pamoja na Umma kwa lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa Vijiji hivyo wanaondokana na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama ambalo limekuwa likiwaathiri kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment